Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Kabwe Zitto ambaye amekitupia lawama Chama Cha Mapinduzi kwa kushindwa kupunguza umaskini nchini
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto ameishambulia CCM kwa kushindwa kuondoa umasikini nchini katika kipindi cha miaka minne iliyopita, licha ya serikali yake kuidhinishiwa bajeti inayoomba kila mwaka.Akichangia hoja ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2010/11 bungeni jana, alisema haijalenga (bajeti hiyo) katika shughuli za maendeleo, badala yake imejikita zaidi katika kuwashibisha watu wenye uwezo na kuzidi kuangamiza walalahoi. “Hii ni bajeti mbaya. Ni kwa ajili ya tumbo. Ina faida zaidi kwa wenye uwezo,” alisema Zitto. Alisema kutokana na ubaya wa bajeti hiyo, watakaoumia zaidi ni walalahoi wanaofikia 13 milioni nchini ambao wanaishi kwa dola moja ya Marekani (Sh 1,400) kwa siku. “Ni bajeti ambayo ina faida zaidi kwa wenye uwezo,” alisema Zitto akichambua kuwa imeshindwa kujitosheleza kutokana na mapato ya ndani. Ili kuendesha nchi kwa bajeti hiyo, Zitto alisema: “Itabidi serikali ikope kwa wahisani kwa ajili ya kulipa mishahara wafanyakazi, kulipa posho na kununua mafuta kwa ajili ya magari”. Akionekana kuwa makini na aliyepangilia hoja zake zilizotiwa na nguvu ya takwimu, Zitto alikigeukia CCM na kusema chama hicho kinapaswa kubeba lawama zote kwa sababu kimeshindwa kutekeleza ahadi zake kulingana na Ilani yake ya mwaka 2005. Kuhusu Chuo Kikuu Dodoma Zitto alidai; "Hilo halipo katika ahadi za CCM, kama yupo mbunge wa CCM asimame aje aonyeshe ni wapi Ilani ya CCM ilipotoa ahadi itajenga Udom, hakuna, hakuna, ‘nachallenge’; kama yupo anayeweza kuonysha aje. Ujenzi wa Udom ni wazo na ahadi ya Chadema ya mwaka 1992". Maneno hayo yaliyomwinua Mbunge wa Ukerewe, Dk Getrude Mongella (CCM) na kuombna mwongozo wa Spika. "Mwongozo wa Spika. Hivi ni utaratibu mzuri kuwaambia Watanzania kupitia Bunge kwamba, CCM ilidanganya", alihoji Mongella baada ya kumyamazisha Zitto kwa kuomba mwongozo wa Spika. Hoja ya Mongella iliungwa mkono na Naibu Spika, Anna Makinda aliyeongoza kikao hicho jana asubuhi. "Upo sahihi Mheshimiwa Mongella, lakinin lazima tukubali kuwa katika wakati huu, ndio wakati hayo yatatokea tu", alisema Makinda. Akichangia hotuba hiyo, Zitto alitumia maneno makali akisema bajeti hiyo ni sawa na barua ndefu ya CCM kutaka kujinyonga kwa kuwa ni ya kuchumia tumbo. " Toka serikali iingie madarakani kwa miaka minne iliyopita Bunge limeidhinisha zaidi ya Sh26trilioni kama bajeti, kutoka 2006/2007 mpaka mwaka 2009/2010. Leo na mpaka Jumatatu tunajadili, na kwa wingi wa wabunge wa CCM kwa vyovyote vile watapewa cheki nyingine ya Sh11trilioni pia. “Kwa ujumla katika miaka mitano, tutakuwa tumewapa jumla ya Sh37trilioni kwa ajili ya kuleta maendeleo, laikini katika miaka minne iliyopita jumla ya Watanzania 1.6 milioni wamekuwa maskini", alisema Zitto. Aliongeza kuwa hadi wakati huu idadi ya watu maskini nchini imefikia 13milioni ambao wanaoishi chini ya dila moja kwa siku, lakini bajeti hiyo ikikaa kimya bila kueleza jinsi itakavyowaondoa katika kadhia hiyo. Alisema bajeti hiyo inatoa faida zaidi kwa watu wenye uwezo ikiwaacha maskini bila ufumbuzi na kwamba, matumizi ya ndani yana pengo la Sh1.8 trilioni, hivyo katika kila Sh100 inayotumiwa, serikali inakopa kiasi cha Sh23. Akichangia bajeti hiyo, DkMongella aliwatuhumu wakurugenzi wa maendeleo wa wilaya kuwa kikwazo cha maendeleo kwa kukosa ubunifu. Alifafanua: “Kupitia Mkukuta (Mpango wa Kupunguza Umasikini na Kukuza Uchumi Tanzania) unaonyesha kwamba utapunguza umasikini nchini kwa kati ya asilimia nane hadi kumi.” Akichangia hotuba hiyo Mbunge wa Tabora Mjini, Siraju Kaboyonga aligusia zaidi sekta ya miundombinu hasa bandari na reli akisema kuwa ipo haja kwa serikali kuchukua hatua za haraka kuliponyesha Shirika la Reli nchini (TRL), alilosema ni sawa na mgonjwa aliyelazwa katika chumba cha wangongwa mahututi. "Bandari zikitumika vizuri zitainua uchumi, tatizo miundombinu yetu, reli, TRL ni gonjwa, lipo ICU, ipo haja ya kuliponyesha haraka. Shirika halina injini, mabehewa mabovu, bado halijaanza kazi licha ya kipande cha reli kilichoharibika Kilosa kutengenezwa. Halina fedha hata za kununulia mafuta. Serikali itenge fedha kulinusuru shirika hili". Alisema Kaboyonga. Wabunge wengine waliochangia mjadala wa hotuba hiyo ya bajeti hadi jana mchana ni pamoja na, Abdalah Mtutura, Juma Killimbah, Mgana Msindai na Chrisant Mzindakaya aliyesema takwimu za Benki ya Dunia (WB)za mwaka 2007 zinaonyesha kuwa asilimia 89 ya Watanzania ni maskini na kuongeza kuwa wengi wa Watanzania ni wavivu. Wengine ni Athuman Janguo na Herbert Mntangi, Khadija Saleh Ngozi ambao walionyesha wasiwasi kuhusu kampuni kubwa za madini kupewa misamaha ya kodi katika mafuta ya kuendeshea mitambo. Mjadala huo wa bajeti unaendelea leo na Jumatatu jioni Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo atahitimisha kwa kujibu hoja za wabunge.
Blog Archive
-
▼
2010
(485)
-
▼
June
(133)
- Brazil 3 – 0 Chile
- We’re only interested in Afghanistan’s stability: ...
- Argentina 3, Mexico 1
- Kangana Ranaut turns to comedy
- USA 1-2 Ghana VIDEO GOALS
- Eminem & Jay-Z Rock ‘Letterman’
- The Saturdays – ‘Missing You’
- Akon's Helpful SRK Tune For Haiti!
- rime Minister David Cameron to hold first sit-down...
- Rapper Eminem honors mentor Dr. Dre at L.A. event
- Ridhawan Kikwete akabidhiwa mikoba ya kusaka wadha...
- MR. 2 a.k.a SUGU AJIUNGA NA CHAMA CHA CHADEMA!!
- MSANII ATANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA ILALA
- Rihanna Upgrades Her Phone With Her Man!
- Enrique Iglesias - I Like It
- President Obama's Statement on General McChrystal ...
- Rihanna - Te Amo
- Selena Gomez
- Alexandra Burke Shoots ‘Start Without You’
- DAWA YA WABAKAJI YAGUNDULIKA
- The Industry Remembers The King
- Trina "Amazin Diary"
- CIARA AND LALA KICKIN IN L.A
- Diddy-Dirty Money – ‘Hello Good Morning Ft. Rick R...
- Tha Dogg Pound - Sky's The Limit
- Alicia Keys' Unborn Baby Blessed By Zulu Tribe
- Raymond Domenech Is No Fan Of Handshakes....
- Argentina beat Greece 2-0
- Shamra shamra za Rais Kikwete kuchuku fomu za kugo...
- Chizika na Joni Woka
- Chizika na Joni Woka
- JK ACHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA URAIS LEO
- Well Now It’s Getting Exciting: Luis Fabiano’s Dou...
- Waka Waka Girl Shakira To Sing For Bollywood
- Justin Bieber - Baby ft. Ludacris
- Justin Bieber - Never Let You Go
- Justin Bieber - Somebody To Love (Remix) ft. Usher
- Dads are usually seen as rule-breakers, risk-taker...
- Sita wajitosa urais Zanzibar, YUMO DK SHEIN, DK BI...
- Kat DeLuna feat. Akon - Push Push
- Is Maradona ‘Messing’ with Messi?
- World Cup rankings: Argentina rises to No. 1
- Spectacular Goals, Anyone?
- IS Shakira to sing a Bollywood cabaret song!
- Kanye West - Coldest Winter
- Megan Fox Engaged again...
- Miles Austin
- Birdman - Loyalty -feat. Lil Wayne & Tyga
- South Africa 0-3 Uruguay
- Alicia Keys wants to adopt child from Africa
- utamu wa bata huu hapa
- kiuno kakupa nani? mama, kiviringishe
- this is how people strugle 4 their life
- Onyx - Shut ‘Em Down ft. DMX
- Obama Speech
- Brazil vs Korea DPR 2-1 - FIFA World Cup 2010
- Brazil Vs North Korea
- Akshay’s Khatta Meetha to be released next month
- Maradona took Argentina job for the cash - Pele
- Hurricane Chris ft The Game, Lil Boosie, Baby, Ang...
- Gucci Mane "911 Emergency
- Gucci Mane - Everybody Looking
- Italy 1-1 Paraguay
- VIJANA CHUO KIKUU DODOMA WAMBEBA KIKWETE KWENDA KU...
- 'acha papara nikikupa utalala'.....mama ntilie - R...
- Trey Songz - Already Taken
- Snoop Dogg ft. Soulja Boy - Pronto
- TFF YAINGIA HASARA MECHI YA BRAZIL NA TAIFA STARS
- Shakira - This Time For Africa
- USA 1-1 England
- Why Diego Maradona is My New Favourite Coach?
- 'Hand of God' offender Maradona's plaintive plea f...
- Bebo song - Kambakkht Ishq
- Zito Kabwe aichapa CCM NA ASEMA ASEMA IMESHINDWA K...
- Shakira - Give It Up To Me
- France, Uruguay play 0-0 draw
- Hivi ndivyo mambo yalivyokwenda...... South Africa...
- Hrithik's Cine Magic With Ash
- Salman-Bipasha end cold war
- chill out 2day by Jody Breeze - Time To Get It Poppin
- KICK-OFF CELEBRATION CONCERT FOR THE 2010 FIFA WOR...
- Biden in South Africa for World Cup 2010
- Mandela’s great-granddaughter killed after World C...
- Shakira -Waka Waka World Cup South Africa 2010
- HOTUBA YA BAJETI YA SERIKALI 2010-2011
- MAMBO YA CHAKACHA (unkula huu )
- Chris Brown New Girlfriend
- Don-Yeh Mera Dil ( Shah Rukh Khan, Kareena Kapoor)
- Shahrukh Khan ~ Sexy and Wet
- Kareena Kapoor is the Best Celebrity Endorser
- Abhishek-Aishwarya get romantic for Lux
- Chris Brown Denied Entry into the UK
- Rosie Huntington-Whiteley: Lovely in Los Angeles
- HAYA NDIO YALIYOTOKEA KTK MECHI YA BRA V/S TAIFA S...
- Kareena Kapoor, Bipasha Basu are friends now
- Arre Re Arre Yeh Kya Huwa -Shahrukh khan
- Ye Ishq Hai - Jab We Met
- Now, SRK snubs Farah Khan
- Hold ON - Sugu ft Andre
- Seriously, What's With all the Girl-on-Girl Kissing?
-
▼
June
(133)