Tuesday, June 8, 2010

HAYA NDIO YALIYOTOKEA KTK MECHI YA BRA V/S TAIFA STARS


Timu ya Taifa ya Brazil imefanya kile ambacho kilitarajiwa na watu wengi au mashabiki wengi wa soka nchini baada ya kuifunga Taifa Stars bao 5-1.Mchezo huo ambao ulihudhuriwa na mashabiki wachache ambao inawezekana labda kutokana na kingilio ambacho kimewekwa na TFF kuwakwaza mashabiki wengi kutokwenda kuishangilia timu yako kutokana na kipato kuwa kidogo.Taifa Stars ilianza mpira kwa kasi lakini Brazil ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kutoka kwa Robinho,Bao la pili limefungwa tena na Robinho na la tatu limefungwa na Remirez,la nne limefungwa na Ricardo Kaka na bao la kufutia machozi la Stars limefungwa na Jabir Aziz kalamu ya magoli ilihitimishwa na Ramirez kwa kufunga goli la tano.Mpaka mwisho wa mpira Brazil 5 Stars 1

HAPA NDIPO TULIPOPIGWA LA TATU

HAPA TULIKUWA TUNAELEKEA KUPIGWA LINGINE

Timu ya Taifa walijitahidi lakini bahati haikuwa yetu kwani tulipata nafasi nyingi sana za kupata magoli lkn nane afunge?

Mshabiki huyu baada ya mpira kwisha alikuwa anamsubiri Dunga kumpa ujumbe wake kama unavyosomeka kwenye bango

Parking ilkuwa imeshiba vya kutosha

Jamhuri kihwelo ina maana uzalendo ulikushinda mpaka unavaa jezi ya Brazil au tukuelewe vipi?

Hatari langoni mwa Stars

Wananchi wengi walikuwa nje kutokana na kukosa kiingilio cha kuingia kuona mtanange huo

Raia wa nje walikuwa wengi kuja kuangalia gemu la kihistoria

Kipindi cha pili kilianza

Wadau wa mpira wakifuatilia kwa umakini mkubwa mtanange huo

Vyombo vya habari vilikuwa vingi sana kuja kuripoti mpira huo

Mashabiki wachache waliohuduria mtanange huo

Hivi ndivyo hali ilivyokuwa uwanjani

hapa tulikuwa tunapigwa lingine...

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisindikizwa na walinzi wake kutoka nje ya uwanja wa Taifa


Dakika za mwisho mwisho mpra kumalizika watu wakiwa hawaamini kilichotokea

Blog Archive