Monday, June 21, 2010

Shamra shamra za Rais Kikwete kuchuku fomu za kugombea urais DOM


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionesha fomu kwa wanachama wa CCM muda mfupi baada ya kuichukua mjini Dodoma leo asubuhi.Pemebeni kulia akipiga makofi ni mke wa Rais Mama Salma Kikwete.
Katibu Mkuu wa Chama Cha mapinduzi Yusuf Makamba akipeana na Rais Jakaya Mrisho kikwete katika makao makuu ya CCM mjini dodoma leo asubuhi,mara baada ya kuchukua fomu ya kugombea Urais.

Katibu Mkuu wa Chama Cha mapinduzi Yusuf Makamba akimkabidhi fomu ya kugombea Urais, Rais Jakaya Mrisho kikwete katika makao makuu ya CCM mjini dodoma leo asubuhi.

Mgombea Urais kupitia CCM Rais Jakaya Kikwete akiwa kwenye hali ya furaha akizingumza na Mzee Msekwa wakati wa zoezi la udhamini mkoani Dodoma likiendelea,kushoto ni Waziri Mkuu Mh Pinda.

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na baadhi ya wanawe wakati Rais Kikwete akichukua fomu za ugombea Rais katika makao makuu ya CCM Mjini Dodoma leo asubuhi(picha na Freddy Maro).

Mama Salma Kikwete na Mama Pinda katika hafla hii
Vijana wa UVCCM wakihakikia kadi za wanachama wanaomdhamini JK
Uhakiki wa wadhamini wa JK waendelea

wengi wajitokeza kumdhamini JK
Uhakiki wa wadhamini wa JK unafanyika kwa makini
Foleni ya wana CCM wanaotaka kumdhamini JK

Blog Archive