kama Bunge, lakini mmoja mmoja kama watumishi wa umma, tunao wajibu mkubwa sana wa kuishi na kutenda kwa mfano. Tujiepushe na tamaa zinazoweza kuliingizia Taifa hili hasara kubwa.
Kauli ya Waziri Mkuu kuhitimisha mjadala wa Richmond,
Mkutano wa 18 wa Bunge, Februari 10, 2010
Mkutano wa 18 wa Bunge, Februari 10, 2010
Haiwezekani kiongozi upende kujilimbikizia mali ili upate umaarufu tu, ni lazima utatumia utajiri huo kuhonga ili kupata kandarasi na mikataba mikubwa...
Sherehe za miaka 33 ya CCM, Mpwapwa, Dodoma.
Februari, 06, 2010
Lazima tuendelee kukataa wenye tamaa ya mali kupindukia... huwa najiuliza sababu za watu kujilimbikizia mali kupita kiasi wakati mwisho wetu wote ni kichumba cha pembe nne....
Sherehe za miaka 33 ya CCM, Mpwapwa, Dodoma.
Februari, 06, 2010
“Tubadilishe tabia, itabidi tujitolee tu kama vile mtu anataka kujiua na tuwasaidie wakulima, wafugaji na wavuvi… katika bajeti tusiulizane, tuelekeze nguvu katika maeneo hayo…”
Akifungua mkutano wa siku tatu wa wadau wa mifugo
mjini Dodoma (Jumatatu, Sept. 28, 2009)
Asilimia 70 ya wakulima nchini hutumia jembe la mkono, asilimia 20 wanyama-kazi na asilimia 10 tu matrekta... Hatuwezi kwenda mbele kwa jembe la mkono. Lazima tulime kwa kutumia zana za kisasa…”
Majumuisho ya ziara ya mikoa ya Mbeya, Iringa na Morogoro kukagua kilimo,
hoteli ya B-Z, Morogoro Mjini,
01 Aprili, 2009
Majumuisho ya ziara ya mikoa ya Mbeya, Iringa na Morogoro kukagua kilimo,
hoteli ya B-Z, Morogoro Mjini,
01 Aprili, 2009
“Tusidanganyane, jembe la mkono halitatufikisha popote kama tunataka kweli kuendeleza kilimo. Lazima tuwasaidie wakulima kikweli kweli,”
Majumuisho ya ziara ya mikoa ya Mbeya, Iringa na Morogoro kukagua kilimo,
hoteli ya B-Z, Morogoro Mjini,
01 Aprili, 2009
Majumuisho ya ziara ya mikoa ya Mbeya, Iringa na Morogoro kukagua kilimo,
hoteli ya B-Z, Morogoro Mjini,
01 Aprili, 2009
“Ma-RC na Ma-DC lazima wapimike. Lazima tuwajue wanasukuma vipi kilimo na elimu ili wakishindwa basi kiwe ni kigezo cha kuendelea na kazi zao ama la”