RAIS mstaafu Benjamin Mkapa amesema kuwa anashangazwa kuona bara la Afrika linaendelea kudhani kuwa litaletewa maendeleo na nchi zilizoendelea hivyo kuendelea kuzitegemea.
Akizungumza jana katika Mkutano wa Kiuchumi wa Dunia kuhusu Afrika kinachomalizika leo jijini Dar es Salam, Mkapa alisema viongozi wengi wa Afrika wanafikiri kuwa ni watu wengine wenye jukumu la kuziletea maendeleo nchi zao.
“Nashangaa sana leo miaka 50 tangu uhuru bado tunategemea wengine watuletee maendeleo? Hili ndio tatizo kubwa ninaloliona kuwa kikwazo cha maendeleo ya Afrika; tunafikiri kuwa ni wengine wenye jukumu la kutuendeleza; tunadhani zipo nchi kwa ajili hiyo hapana; sasa tubadilike. Njia ya kubadilika ni kukubali kubadilika,” alisema Mkapa.
Huku akionyesha msisitizo na kuchukizwa na hali ya kutegemea misaada, Mkapa, ambaye pia ni kamishna wa Tume ya Afrika iliyoanzishwa na aliyekuwa waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Tonny Blair mwaka 2004, alisema inashangaza zaidi kusikia kiongozi akizungumzia maendeleo anauliza ni wapi au nani atampa fedha na kushindwa hata kufikiria kukopa.
“Inashangaza zaidi, kukuta viongozi wa Afrika wanazungumia maendeleo ya nchi zao, lakini mnauliza ni nani atampa fedha; ni wapi tutapata na wala si kuazima, huu ni ugonjwa,” alisema Mkapa ambaye ni mmoja wa makamishna wa tume hiyo iliyofanya kazi ya kutafiti sababu za Afrika kushindwa kuendelea.
Alisema: “Wakati umefika; simameni kwa miguu yenu; jipangeni na tembeeni kwa miguu yenu, utegemezi ni ugonjwa mkubwa katika Afrika; Tuwe Waafrika”.
Mkapa alitoa mfano wa waziri mkuu wa Ethiopia, Meles Zenawi kuwa anafaa kuigwa katika Afrika kwa kuwa na mawazo, mipango na mikakti inayojitegemea kwa ajili yake, nchi na taifa lake.
“Siwezi kujizuia naomba niseme nampongeza Melesi Zenawi, waziri mkuu wa Ethiopia kwa kuwa ni mfano wa kuigwa kwa kuwa anafikiri kwa kujitegemea kwa ajili yake na kufanya mambo kwa kujitegemea,” alisema Mkapa.
Rais huyo mstaafu alikwenda mbali zaidi na kusema kuwa Afrika inategemea kuendelea kwa misaada ya nchi za Ulaya ambazo alisema zinatoa misaada kwa lengo la kuzitawala nchi za Afrika ambazo zimesahau kuwa zilipata uhuru baada ya kuudai kwa nguvu kutoka nchi hizo za Ulaya.
“Tulipambana kudai uhuru kwa kuwa tulijua tukikaa kimya hawatatupa uhuru; tukapiga kelele hata kutumia nguvu ndipo kutapata uhuru.
Sasa itakuwaje hao waliotupa uhuru kwa nguvu watuletee maendeleo? Haiwezekani wao wakoloni wakitusaidia, wanawaza kututawala; tuachane nao tusimame kwa miguu yetu,” alisema Mkapa.
Mkapa anayeongoza pia taasisi yake ya Mkapa Foundation inayojuhusisha na mapambano dhidi ya Ukimwi, alisema bara hilo pia lina tatizo la kuiga kila jambo kutoka Ulaya, lakini kushindwa kuyafanyia kazi.
Alibainisha kuwa rafiki wa kweli wa maendeleo ya Afrika ni China ambayo alisema haina uhusiano na ukoloni bali wanafikiri juu ya uhusiano, biashara na maendeleo.
“China hawana uhusiano na ukoloni, hawa ni wenzetu, hawafikirii kututawala bali wanataka maendeleo na biashara,” alisema.
Awali Waziri mkuu wa Ethiopia alitaja sababu zinazoifanya Afrika isiendelee kuwa ni pamoja na kukosa miundombinu, rasilimali watu na utawala bora.
Blog Archive
-
▼
2010
(485)
-
▼
May
(82)
- Pankh Movie Reviews
- Kareena Kapoor to feature in Fifa World cup 2010
- CHIILL OUT...Sean Kingston & Detail - Rude Girl
- Banjuka na song la week end.. from Tyga - G Shit ...
- Usher - OMG
- Wagosi wa Kaya na simu za mkononi
- check out ...this clip...
- chill out with ........P Square More Than A Friend
- TAIFA STARS KUCHEZA NA BRAZIL TAR 7 JUNI
- Gyaneshwari Express derails, hit by goods train in...
- Brazilians arrive in South Africa for World Cup
- At $5 mn, Obama 'poorest' US Presidents in 57 yrs
- Bonta - Nauza Kura Yangu ....tanzania mwaka huu tu...
- IS 24 TV SERIES ENDING SEASON 8?
- Animation is not fun
- Photoshop, digital paintingThis was done in photos...
- [flash] Flash animation
- Watch out clip from Rihanna - Rockstar
- Chill ..chill out...Yukmouth - The Hard Way (feat....
- Chill out with this clip from Tyga & Chris Brown -...
- Bio of Mary Lynn Rajskub who plays Chloe O Brian i...
- GET LINK FOR 24.S08E23 and 24
- LIYUMBA ATUMIKIA MIAKA 2 JELA
- Check out this clip Bob Sinclar & Sahara ft. Shag...
- Xplicit Lyric - I'm Nice Wit It
- check out the clip Sterling Simms - Boom Boom Room
- [video] pixilation of french fries (animation)
- [photoshop] invisible man
- DAKIKA IO ZA ZINADINE ZIDANE
- Taio Cruz - Break Your Heart ft. Ludacris
- [3D model] Robot model
- check out this clip fromTimbaland - Carry Out ft. ...
- KOMBE LA DUNIA SOUTH AFRICA 2010 MAENENEO MBALIMBA...
- Air India Crash today may 22 ,2010
- [3D model] Lancer Evo X modeling
- Style showdown; 90210's_jessica_stroup V/S Glee's ...
- Is something wrong with katrina's lip????
- Ranbir kapoor Deepika padukone khuda jaane bachna ...
- chizika from india Aaja Mahiya - Roshan
- "Heroes" Headed for Abrupt End?
- AMITHA BACHCHAN WA BONGO 'JB' AJA NA FILAMU YA 'S...
- CHECK THIS CLIP FROM ACTRESS NAMITHA
- Vampire Diaries Babe Is Team True Blood
- 24.S08E22
- Priyanka Chopra with Akshay Kumar movie Andaaz
- check bollywood song from Don film Don-Yeh Mera Di...
- THE GREATEST NA JACKLINE WOLPER WAJIACHIA KWENYE S...
- SHEREHE YA KUWAAGA WAHITIMU 2010 TSA HYDERABAD YA...
- T.I. 1st Interview since he was released from pri...
- Diddy-Dirty Money - Hello, Good Morning (feat. Ric...
- THE VAMPIRE DIARIES S01E22
- CHECK THIS CLIP Sean Kingston
- Sean kingstone atinga ndani ya studio za Clouds FM
- Sean kingstone kuanza makamuzi vilivyo jmosi diam...
- [flash tut ] Oval Tool
- [flash tut ] Line Tool
- Sean kingstone awasili Dar kuwakonga wabongo kweny...
- QUOTE MBALIMBALI ZA MTOTO WA MKULIMA TANZANIA
- [flash tut ] Lasso Tool
- [flash tut] ] Ink Bottle tool
- PATA TELEVISHENI ZA AFRICA ONLINE KUPITIA HII SOFT...
- Lady GaGa - Telephone (ft. Beyonce)
- T.I IS BACK........LISTENING HIS TRACK i m back
- CHECK OUT THIS CLIP Ciara - Ride (ft. Ludacris)
- Britain's David Cameron becomes PM; Brown out
- MKUTANO WA KUJADILI SHEREHE YA WAHITIMU TSAH 2010 ...
- Chizika na TANZANIAN Bongo flava ...Angie with My Boo
- Manchester United Striker Wayne Rooney Named Barcl...
- HAYA NDIO MAMBO YA PRESI OBAMA
- M/KITI KAMATI YA KATIBA TSAH INDIA
- Star Beyonce in Tanzania with African beauties
- New York City The capital of the world
- Historical site of kaole Ruins in Bagamyo region,...
- Tanzania Prime Minister's Profile (peasant’s son)
- 24 SERIES JACK BOUER/KIEFER SUTHERLAND
- TANGAZO LA MKUTANO WA WAHITIMU TSAH INDIA
- MKAPA ASHANGAZWA NA NCHI ZA AFRICA KUTEGEMEA MISAA...
- Ajmal Amir Kasab Pakistani terrorist given Death S...
- MTOTO WA MKULIMA AANZA HOTUBA YAKE KWA WIMBO WA LU...
- KATIBU MSTAAFU TSAH BW. ABDALLAH MBAROK AREJEA NY...
- Trap Or Die 2, Mixtape Young JeezyLatest Updates...
- Katibu mstaafu wa jumuiya ya tsah mwaka 2008/9 Bwa...
-
▼
May
(82)