Maandamano ya wanaosadikiwa kuwa wanachama na wapenzi wa CHADEMA yakikatisha mitaa ya jiji la Arusha muda mfupi uliopita
Polisi wayapiga stop maandamano hayo
Maandamano yakiwa yamepigwa stop
Maeneo ya unga limitedMh. Freeman Mbowe akizungumza na Tanzania Daima kutoka Arusha jana jioni alisema maandamano hayo yatakayohitimishwa na mkutano mkubwa wa hadhara, ajenda yake kuu ni kupinga hatua ya serikali kuvunja sheria kwa makusudi na kukipa Chama cha Mapinduzi (CCM) ushindi ulio kinyume cha sheria katika uchaguzi wa umeya uliofanyika hivi karibuni.
Mbowe akizungumza na Tanzania Daima kutoka jijini Arusha jana jioni alisema CHADEMA itaanza rasmi kuitumia nguvu ya umma kupinga kile alichokiita "uhuni uliofanywa na CCM na serikali yake kujipa ushindi wa lazima katika uchaguzi wa umeya kinyume na matakwa ya sheria halali za nchi.
"Mwanza hakujafanyika uchaguzi kwa sababu ya dhuluma, Kigoma na Arusha uchaguzi ulikuwa batili kabisa. Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) tumemsihi sana aingilie kati lakini ameendelea kushirikiana na chama chake (CCM) kuinyima CHADEMA haki ya kuongoza. Tunakwenda kulaani kwa nguvu zote uchakachuaji wa maamuzi ya wananchi" alisema Mbowe. Kwa chanzo na habari kamili....

