Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dr.Ali Mohamed Shein akiwashukuru wajumbe wa Halmashauri kuu ya taifa CCM kwa kumchagua kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza makamu wa Rais Dr.Ali Mohamed Shein kwa kuchaguliwa na wajumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM kuwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi katika ukumbi wa White house mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo.
Mwenyekiti wa CCM ,Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza kikao maalumu cha Halmashauri kuu ya taifa CCM kilichompitisha Dr.Ali Mohamed Shein kuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Dr.Gharib Bilal kwa kukubali matokeo ya ushindi wa Dr.Ali Mohamed Shein kuwania urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM
Mwanasiasa Mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru akimpongeza Dr.Gharib Bilal kwa kukubali matokeo ya uchaguzi ambapo Dr.Ali Mohamed Shein aliibuka mshindi katika ugombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM mjini Dodoma.
Dr.Mohamed Gharib Bilal akimpongeza Dr.Ali Mohamed Mohamed shei kuchaguliwa mgombea Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM mjini Dodoma.
Baadhi ya wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa CCM wakiwa katika kikao maalum kilichompitisha Dr.Ali Mohamed Shein kuwa mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi usiku wa kuamkia leo mjini Dodoma
DR.SHEIN ALIWASHINDA GHALIB BILAL AMBAYE AMEPATA 54 NA KUSHIKA NAFASI PILI AKIFUATIWA NA SHAMSI VUAI NAHODHA AMBAYE AMESHIKA NAFASI YA TATU KWA KUPATA KURA 33 HABARI NDO HIYO WADAU.
HATIMAYE MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DR. ALLY MOHAMED SHEIN AMEIBUKA KIDEDEA KWA KURA 117 NA KUWABWAGA WAPIZANIA WAKE DR. GHALIB BILAL NA WAZIRI KIONGOZI WA SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR SHAMSI VUAI NAHODHA KATIKA KINYAG'ANYIRO CHA KUWANIA KUGOMBEA URAIS KISIWANI ZANZIBAR.
DR.SHEIN ALIWASHINDA GHALIB BILAL AMBAYE AMEPATA 54 NA KUSHIKA NAFASI PILI AKIFUATIWA NA SHAMSI VUAI NAHODHA AMBAYE AMESHIKA NAFASI YA TATU KWA KUPATA KURA 33 HABARI NDO HIYO WADAU.