NA.RAITON M.AMBELE
Aahaha basi TONNY umenikumbusha Professor wangu wakati wa somo fulani la Uchumi wakati wa fall spring semester mwaka huu...Darasa lake la kwanza kabisa na wanafunzi alizoa mzozo mkubwa saana darasani na huku akiacha wamarekani weusi wakitishia kumpeleka kwenye management kwa kile alichikiita IQ and intelligence among different ethnics!!Kutoka na research ambazo zimefanywa, sub saharan africa inashika mkia kwenye kuwa na akili ndogo, huku kabila dogo kutoka kaskazini ya Israel wakilamba asilimia 95 na kushika nafasi ya kwanza....Ndipo mzozo kutoka kwa wanafunzi ukaanza huku wakitaka kujua ni sababu zipi zimepelekea waafrica kushika mkia, na yeye professor akaanza kuzimwaga sababu kadhaa ahaha! siwezi kuzitaja adharani ila naweza kuwapa link kadhaa ya research papers...Kijana mmoja kutoka Ethiopia akapinga vikali study hiyo, sasa katika pitia pitia ya research darasani tukakuta ethiopia walikuwa wanakaribia kushika mkia huku wakiambulia asilimia 36, Tanzania tukiwa juu yao!!!Mzozo ulikuwa kubwa saana, robo darasa ikabidi wadrop darasa lake...lakini yeye aliendelea kushika uzi ule ule kuwa kama kuna mtu anapinga study hiyo basi aandike term paper( hizi ni reseach ndogo kwa wanafunzi wa masters) kuhusu IQ, kijana wa ethiopia ilibidi aape kuandika paper kupinga study hiyo, sasa alama alizopata sijuhi ( ahaha)....Ilikuwa vita vuta ni kuvute, je ni kweli waafrika tuna akili ndogo? na je ni kwanini tuna akili ndogo? kuna wakubisha? je akili ndogo inatokana na nini?I have good articles, anayetaka naweza kumpa link, ila mh! sometimes huwa nakubalina kuwa..." NI KWELI WAAFRIKA TUNA AKILI NDOGO"....
Tarehe: 25/11/07 1:12 AM, KapongolaNimefurahishwa na makala hii, naomba hiyo link kwa maarifa zaidi. Email yangu ni kapongola@yahoo.com Tarehe: 25/11/07 2:20 AM, Anonymoushuyo baba naye jinga tu . Hivi anajua hakuna mtu mweupe na mweusi? kuna wengine ni yellow, wenginde dark tan sasa nao akili zao zipo vipi...? asitake nimtukane mimi sasa hivi na nobel yake...Tuemtawaliwa toka tujulikane ulimwenguni huu...Walioletwa mateka mpaka leo uhuru wao ni wa vitabu tu lakini the reality kazi atapewa mzungu lakini black america itachukua muda.Africa walitunyanyasa na kutufanya vijakazi wao...wametupa uhuru ukaja na madeni kila siku...tunalipa madeni yasiyoisha kila siku interest juu...na madeni ya sheria....huyo baba sijui vipi...hiyo nobel basi ameona kila mtu mjinga but him Tarehe: 25/11/07 6:35 AM, Anonymouskaka Mjengwa,kuna hata ushahidi kabisa kuwa mtu mweusi ni mtu mbumbumbu zaidi duniani hata kufikiriDr Samwel Cartwright aliyeishi nchini USA enzi za bishara za utumwa ndiye alikuwa mtaalam wa kwanza kufanya reaserch kwa miaka 21 na kuja na jibu kuwa mweusi IQ yake na ujazo wa ubongo wake ni kidogo kwa asilimia 10 dhidi ya mweupeDr Cartwirgt akaendelea kuwa uwezo wa kufikiri wa mtu mweusi upo kidogo kwa sababu ya mafuta mengi ndani ya ubongo yanayomfanya awe anatoa maamuzi ya ajabu na kuji-behave kusikokuwa kwa ubinadamu ambaye yeye akaita kitaalam kama"DREPOTAMINIA",na akaendelea kuwa ndiyo maana hata mweusi anaweza leo akakataa sehemu nzuri akaenda sehemu mbaya kwa sababu ya uwezo mdogo sana wa kufikiri,yeye akaita hali hii kama"DYSENTIASIS ETHIPOISIS"uchunguzi huu wa Dr Cartright ukaja kuungwa mkono na daktari mwingine baadae aliyefanya nae reaserch yake kwa muda mrefu kuhusu uwezo wa akili ya mzungu na mweusi,huyu si mwingine bali ni dr Morton G,yeye liongeza kuwa IQ ya mweusi ni ndogo sana kiasi kwamba hawana uwezo wa kujua hili lina faida kwa jumuia na hili halinaKwa jinsi ilivyo,na akili zao hasa hawa viongozi wetu wa Kiafrika hata mimi nakubali kuwa sisi waafrika tuna laana na uwezo wetu wa akili sio tu kama umezidiwa na wazungubali kila races hapa dunianiiweje mtu kama Abacha wa Nigeria aibe hela ambazo hata yeye na familia yake tena wanunue kila kitu wanachokitaka hawezi kumaliza labda ka miaka elfu 2000?Iweje Rais kama Campoire wa Bukinafaso aue wenzake kwa sababu tu ya madaraka?iweje Rais wa Kabila wa Congo aingie mkataba na Ublgiji kuwa wao wachukue madini kule Katanga,na in return congo ipate bunduki aina ya SMG kuwadhibiti wasi wa kibanyumulenga kusini mwa nchi hiyo?iweje JK na kaka Karamagi wasaini mkataba mfu wa BUZWAGI,iweje mtu mwenye akili asaini mkataba wa ajabu wa Buhemba ambapo eti mwekezaji atalipa kodi miaka 10 baada ya kuanza kuvuna madini tena kwa asilimia 3?Sasa wazungu wakisema tena kwa ushahidi wa maabara kama sisi tuna akili finyu tena kw amifano anuai kwa nini tunalalama?NI KWELI NA NAKUBALIANA NAO,WAAFRIKA NIKIWEMO MIMI NA WEWE TUNA AKILI FINYU!! Wewe mtz unayesoma nakala hii,,umemfanya nini JK anapoingia mikataba ya ajabu kama vile TZ ni nchi yake binafsi na mwenzake Lowassa?umemfanya nini Mkapa aliponunua ndege ya kifahari sana huku watu hata kwao Mtwara wanakufa kwa njaa?umefanya nini wanafunzi chuo kikuu walipofukuzwa kwa serikali kushindwa kulipa milion 980 kama ada kwa wanafunzi kwa mwaka huku IKULU ikipewa milion 3000 kila mwaka kwa sababu ya matengenezo yasiyokwishaikishinda hata bajeti ya USA congress inayoipa Ikulu yao kwa kazi hiyo?Umefanya nini wewe binafsi kumpinga Mkapa kwa kununua rada yenye thamani ya bilion 40 ikiinda hata mojawapo ya nchi ya kwanza kwa uchuni sasa barani Afrika Libya ambayo rada yao ni nafuu zaidi"Hakuna haja ya kulalamika,ni kweli sisi waafrika hatuna uwezo mzuri wa kufikiriJK anaendelea kuvunja katiba,na wanaomsema wananyanyaswa na serikali bila sisi watz kumkemea,,je ungekuwa ndiye wewe yule mtoto wa Mwamza aliyemuuliza Lowassa swali la msingi la kikatiba hasa kwa nini JK anavunja katiba kwa kumteua mbunge wa Tabora Dr Mseleka kuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza,ungejisikiaje kwa kunyanyaswa na wana usalama kisa tu umeuliza sawali hilo"gumu"kwa wakuu hawa?je hakuna kati yetu watz milion 40 sasa tena wenye elimu si haba wanaweza kuwa wakuu wa mikoa/wilaya bila kuwa wabunge?Ni haki kwa MTZ mmoja kuwa mbunge,Waziri,mjumbe wa kamati ya bunge ndani ya bunge,mwenykiti wa bodi,mwenyekiti wa Tume aliyeteuliwa na Rais,mjumbe wa CCM-NEC,mjumbe wa kamati kuu ya ccm,na mlezi wa chama cha Maskauti tzKwa nini kama tuna akili timamu hatuyapingi haya kama wenzaetu tunavyoona wakipinga kwa kupitia UTAIFA wao?naam ni kweli na tusibishe,sisi hatuna akili!! Tarehe: 25/11/07 4:13 PM, KapongolaSuala la wazungu kuwa na akili kuliko waafrika (weusi) linaweza kua na punje ya ukweli ndani yake. Na mie nimejaribu kujadili hili na baadhi ya watanzania wenzangu na nilichopata kutoka kwa wengi ni ushabiki.Kwangu mimi akili inaweza kutafsiriwa ni uwezo wa kutambua mazingira yanayomzunguka binadamu na kuweza kutumia vitu vinamvyomzunguka kutafuta suluhisho ya matatizo yanayomkabili. Tunaweza kujadili katika hili.Wengi niliowahi kujadili nao waliona hili sio suala la kujadili kwani, linamdhalilisha mtanzania (mweusi) kwa upande mmoja na pia kukinzana na maadili ya dini kwa upande mwingine. Hivyo wengi wao (watu niliofanya nao majadiliano) hawakufikia kutoa sababu kwanini wanafikiri au kuamini vinginevyo.Katika utamaduni wa mtanzania pamoja na aina ya elimu tuliyopata inakua vigumu sana kujadili suala kama hili.Pengine nitoe sababu zangu zinazonifanya nipate punje za ukweli katika maneno ya James Watson. Ukiangali historia, wazungu ndiyo walioanza kuendelea kwa upande wa kurahisisha upatikanaji wa mahitaji muhimu ya binadamu. Wapo watanzania waliotoa sababu kwa hili kwa kusisitiza kua wazungu walikua katika mazingira magumu hivyo iliwapasa kutafuta unafuu. Mie pia nina swali hapa ambalo pengine linaweza kuleta ulinganisho kwa upande wa mtu mweusi. Tangu lini mtu mweusi amekua anakabiliwa na matatizo ya kupata mahitaji muhimu ya maisha kama vile chakula, mavazi na malazi? Na pengine unaweza kwenda mbali zaidi, ni lini mtu mweusi alifikiria kuendeleza kile alichonacho kiwe bora zaidi? Hapa nazungumzia ubunifu (innovation). Kwa ulingisho tu, ni vitu vichache sana vimebuniwa na watu weusi ukilinganisha na vile vilivyobuniwa na wazungu (magari, computer, meli, ndege na orodha inaweza kujaa ukurasa huu. Kwa lugha nyepesi, tujaribu kuangalia vitu mtanzania wa kawaida anavitumia kwa siku na kuviweka katika makundi mawili tofauti, moja vilivyobuniwa na wazungu na linguine tulivyobuni watu weusi. Mtu mweusi amekabiliwa na maisha duni (umaskini) kwa karne kadhaa hadi sasa lakini hakuna lolote linalofanyika kuleta suluhisho. Hili nalo linahitaji akili kufikiri kupata suluhisho kwa wakati uliopo kwa kuzingatia ukinzani unaowezekana kuwepo kutoka nje. Ndugu zangu ambao nimewahi kujadiliana nalo hili wanajitetea kua wazungu wameendelea kwa kua walitutawala. Kwa mawazo yangu, ile hali ya kutawaliwa tu ni kielelezo tosha cha kupungukiwa akili ukilinganisha na yule mtu aliyekutawala.Utetezi mwingine unakuja kwa kusema mbona watu weusi wanaweza kufaulu mitihani kuliko wazungu wa darasa moja. Kwangu mie hii sio akili kwani kwa kuangalia tafsiri ya akili. Pia inategemea huo mtihani ulihusu nini kwani mingi ya mitihani tunayofanya inapima jinsi ya kueleza yale tuliyofundishwa. Kwangu mimi akili imejikita sana katika uvumbuzi, hivyo ulinganisho unaweza kuangalia ni vitu gani watu weusi na weupe (wazungu) wamegundua hadi sasa.Majadiliano ya suala hili ni marefu, ila kwa leo ningependa kuishia hapa. Kapongola@yahoo.comDortmund, Germany Tarehe: 25/11/07 5:04 PM, ANALYSTHuu ni wakati wa mtu mweusi kupinga hoja hii kwa vitendo. Siyo kwa kutumia majukwaa ya kisiasa au ya haki za binadamu kama ambavyo tumekuwa tukifanya kwa karibu miaka mia moja sasa. Kwa maoni yangu, haya hapa chini yanawezekana kwa kila nchi. Tukumbuke hoja hupingwa kwa hoja siyo kwa kelele.1. Tubadili sheria ZOTE za kikoloni zinazotufanya tudharau vya kwetu na kuwa watumwa wa uvumbuzi "innovation" ya wengine. Kwa mfano, sioni sababu ya kuzuia wataalamu wa kutengeneza bunduki za kienyeji "gobole" kuwa eti ni kosa la jinai kutengeneza silaha "ammunition". Wataalamu hao waendelezwe, bidhaa zao zithaminiwe ikiwa ni pamoja na madawa. Kama leo amebuni gobole kesho atabuni rada na baada ya muda, wamarekani na maadui zao watanunua silaha kutoka kwetu.2. Bajeti kubwa iwekwe katika tafiti za kisayansi. Kila anayeonekana ana kipaji fulani aendelezwe. Vyuo vya kati viwe vingi zaidi kuliko vyuo vikuu. Historia inaonyesha wavumbuzi wengi wanapikwa kwenye politechnics, siyo vyuo vikuu. Wasomi wa vyuo vikuu wana tafsiri innovation na kuboresha zaidi. Kwa mfano ni rahii zaidi kwa kijana wa veta kubuni toroli mpya kuliko mtu wa chuo kikuu. Tusidharau vyuo vya kati kwa kukariri kuwa tunahitaji wasomi wengi. Wa kazi gani kama hawana jipya?3. Umangimeza "bureaucracy" katika mashirika mbalimbali na idara za serikali utokomezwe. Watu wasirundikiwe madaraka. Hili ni kosa KUBWA MNO! Tunashindwa kutumia vipaji vya watu wengine kwa kuwa tu tumekariri kuwa fulani na fulani wana uwezo huu.Yeye yeye ndiye mbunge, mkuuwa mkoa, afisa nini na nini. Nimesoma maoni ya ANON hapo juu kuhusu hili na amenigusa sana. Nafikiri hivi ni viashiria vya umbumbumbu wa viongozi na wanachi kwa ujumla. Natamani kufanya kampeni ya theory mpya ya mgawanyo wa majukumu barani Afrika.Tuna watu wengi sana badala ya kuwa stepping stones wamekuwa road blocks katika kuleta maendeleo na nadiriki kusema WANAABUDIWA. Kama unabisha kuwa siyo wana abudiwa, inakuwaje watu hao hao, hawana jipya, kila siku utawakuta na tai zao wanapigiwa makofi na kusifiwa njaa, umasikini, ujinga na kila aina ya zahma zinatuandama wao wapo tu! Huku siyo kuabudu sanamu? Kwanini katiba isiseme qualifications za watu kushika majukumu ya kitaifa na kuwapa muda kuonyesha matokeo? Hili linanikera sana, naomba nisiendelee nitaacha hoja ya msingi.4. Tuache unafiki kuhusu dignity ya mtu mweusi. Ni kweli tumeonewa vya kutosha, tumepuuzwa vya kutosha na tumedharauliwa vya kutosha. Sasa lazima tujikomboe. Hoja kama vile UZAWA na kumpa upendeleo maalum mtanzania MWEUSI lazima zikubaliwe na kila mpenda haki. Huku kukaririsha watu ujinga kuona kila kitu critical ni ubaguzi wa rangi ni umbumbumbu. Walioishi ulaya na Marekani wanjua kuwa wasio wazawa wa asili wa nchi husika mpaka leo hawana fursa sawa na wenzao walio wazawa.analystmunge@yahoo.com Tarehe: 26/11/07 12:28 AM, MlalahoiWanakijiji,Nimekuwa nikisoma makala zenu, na zinazidi kunipa mwanga zaidi, makala yako Kapongola inanipa mwasha washa wa kuandika tena, ingawa sikubaliani na mwanakijiji anayejitambulisha kama ANALYST!Waafrika kuwa na akili ndogo haiendani na "gene" genetic inheritance, na wala haina uhusiano wowote na kutawaliwa na wakoloni...Makala ya anonymous aliyemtangulia Kapongola ina maswali ya kujiuliza na mimi nayaona kama yana msingi imara!Narejea kwenye mada yangu kama nilivyoanza kabisa kuchangia mada hii pale mwanzo....hainijii akilini kuhusisha suala la akili ndogo na dini au kutawaliwa na ukoloni...uwa napata wakati mgumu pale darasani professor akianza kuchangia mada za kuzolota kwa uchumi wa mwafrika, huwa natamani nitoke darasani kwa kuona AIBU tupu...Kutawaliwa kwa mkoloni haiwezi kuwa kigezo kama wanasiasa wanavyopanda jukwaani na kuanza kudai! Tujiulize, ni mataifa mangapi ambayo yametawaliwa na sasa yako juu kiuchumi...Nitoe mifano kama Marekani ilishatawaliwa na kupata uhuru wake 1777 kama sikosei, Hong kong na singapore ni makoloni ya mwingereza mpaka kalne ya 20, sasa wako wapi?Tanzania tumepata uhuru 1961, ni miaka 46, ni umri wa mtu mzima! bado tunasimama mbele za majukwaa, na pengine tunaingia darasani na kuanza kuambiwa wakoloni walidumaza maendeleo yetu!Nenda Economic Forum, WB, IMF or UN simama uanze kuwaambia watu (toa lecture) kuwa Tanzania haipati maendeleo kwasababu ya kutawaliwa na mkoloni, unaulizwa lini wakoloni waliondoka nchini kwako unasema 1961! still bado unasingizia kutoendelea kwasababu ya ukoloni!???Let be serious, 45 yrs!!! mkoloni aliondoka na ardhi, raslimali zoote? does those resources renewable or not?Wanakijiji, miaka 46 ya uhuru bado mtoto anakalia matofali darasani, hospital haina chandarua, ziwa voctoria halijakauka lakini mzalendo wa pale Kashai Bukoba mjini, Nyegezi mwanza, Kahama shinyanga HAWANA MAJI!!!?? KISA? mkoloni aliondoka na maji ya lake victoria!!!!!?Ni bajeti ipi inaelekezwa kwenye miundombinu ya kumwezesha mtanzania apanue akili yake, akili iwe zaidi ya sasa? Je si kumpatia elimu bora, je si kuwekeza katika kumpambana na maradhi? je si kumpatia lishe bora? Je si kumkinga na magonjwa ambayo yaweza kuepukika?Bunge linakaa, mchangiaji anatumia si chini ya dakika 5 kati ya 10 alizopewa kuchangia yeye anatumia muda mwingi kumpongeza mke wa waziri kuanzisha duka, anatumia muda mwingi kuorodhesha wapiga kura waliomchagua kuanzia ngazi ya kijiji hadi mkoani LAKINI ANASAHAHU KUWA MUDA ALIOPEWA SI KUTOA SHUKRANI NI KUCHANGIA MADA MBADALA YA KULETA MAENDELEO! Leo wanakijiji na wasomi wanadiriki kuandika kwenye blog mbalimbali eti tunasingiziwa tukiwambia tuna akili ndogo!!!!!Naweza andika mpaka kesho!!!! Tarehe: 26/11/07 3:16 AM, ANALYSTKwako Mlalahoi,Umesema hukubaliani na mwanakijiji aliyejitambulisha kama ANALYST ila hukusema hukubali nini na kwa nini. Ukinijulisha hukubali nini, nitarejea na kufafanua. Umepinga sana swala la kutawaliwa. Mimi pia silihusishi moja kwa moja na IQ ila nalihusisha MOJA KWA MOJA na magumu yanayotukabili watu weusi duniani haswa wanaoishi barani Afrika. TOFAUTI na Marekani na nchi za Asia zilizowahi kutawaliwa kama sisi waafrika, wao WALIPATA UHURU KAMILI na waka RUHUSIWA kuwa huru. Kimsingi Afrika bado haiko huru, nikiwa na maana ya uhuru wa kiuchumi. Wenzetu wanaelewa wakitupa uhuru huu, baadhi yao watakuwa masikini kama sisi. Huu unyonyaji lazima uendelee ili watu wa magharibi waishi maisha wanayotaka. Sasa hivi duniani kuna kambi mbili tu kubwa WATU WEUSI na WAZUNGU. Utafiti huu wa akili ndogo, haujasema Waasia au Waarabu au wachina, ni BLACK MAN!! Kuzijua kambi hizi soma kitabu cha "The White Man's Burden" weka hiyo title kwenye mtandao wa Amazon kwa kuwa uko US kwa masaa 8 tu utakipata. Ni kweli Wamarekani walitawaliwa,walipopata uhuru wakaanza kutawala wengine na sasa wanatutawala. Soma kitabu cha "The Confession of an Economic Hitman" Wazungu wenzao, yaani Waingereza walio watawala, waliwapa uhuru kamili. Sisi ukoloni mamboleo bado upo mpaka bafuni, wanalosema ndilo tunalotenda. Kabla ya "uhuru" tulikuwa tuna tawaliwa na taifa moja Uingereza. Baada ya uhuru tunatawaliwa na mataifa karibu yote ya magharibi yakiongozwa na Marekani kwa kushirikiana na WB na IMF. Kuna conscipiracy inaendelea lengo lake ni kuendelea kulipora bara la Afrika kiuchumi. Watu wengi hawakubaliani na mimi ninaposema tunahitaji "rethinking the dignity and priviledges of African people in their own land". Ninahitaji "rethinking" miongoni mwa wasomi na wanasiasa kuwe na upendeleo wa wazi kwa mtu mweusi kiuchumi!! Kupewa mikopo, kumilikishwa makampuni, kuuziwa hisa na kupandishwa cheo. Tusikaririshwe kila kitu ni ubaguzi wa rangi, no way!! Lazima Watanzania kwa mfano, tuwe na sera inayofanana na "Affirmative Action" (Marekani) au "Black Empowerement" Afrika kusini. Tuwatafute kina Idd Simba popote walipo watueleze namna ya ku "take risk" kumkomboa mwafrika katika nchi yake. Mkiendelea kuwaogopa Waasia kwa kuwa wanawapa pesa za kufanyia kampeni mtawabinafsishia kila kitu mpaka nchi nzima iwe yao. Mkiendelea kuwaogopa wazungu "wawekezaji" wataendelea kuchota madini na kuacha mashimo. Lazima jitihada za makusudi zichukuliwe kumpendelea mwanchi wa kawaida. Kinyume na hapo umasikini utazidi, watoto wetu watendelea kukalia matofali, kukosa elimu na kushindwa "kufikiri" mwishowe tunaambiwa hatuna IQ ya kutosha. Ukombozi uanzie katika uchumi. Tarehe: 26/11/07 6:05 PM, Jaduong MettyWandugu,Hizi hoja za IQ nimejaribu kuzijibu. Hebu nitembelee hapa:http://mettyz-bongoland-reflections.blogspot.com/2007/10/rtf-white-intellectual-supremacy-no-way.htmlHalafu, nenda na hapa vilevile:http://www.slate.com/id/2178122Kwa kifupi, intelligence ina sehemu kuu mbili: "nature" na "nurture". Ya kwanza ni akili ya kuzaliwa na sehemu ya akili zetu zinatokana na mazingira. Kwa mtazamo wangu, tatizo la waafrika ni mazingira zaidi ya chochote kile. Na mazingira inajumuisha tamaduni, attitude, etc Tarehe: 27/11/07 10:06 PM, AnonymousNapenda kurudi tena kwani hoja za ANALYST zinanitia mashaka kidogo. Napenda kumweleza kua, watu weusi tungefanikiwa kudhihirisha ukubwa wa akili zetu kwa kuwaondoa wakoloni na kuwafanya watupe uhuru kamili. Nashangaa sana watu tunaposema "kama tungepewa uhuru wa kweli tungekua mbali sasa" badala ya kusema "kama tungetafuta uhuru wa kweli sasa tungekua mbali. Watu weusi tunapokuwa na haya mawazo ya kuangalia kwanza tunafanyiwa au tutafanyiwa nini badala ya kuwa na mawazo ya tunafanya nini au tutajifanyia nini tunazidisha nguvu ya hawa wataalamu wanaosema kua akili zetu ni ndogo. Kama si kweli akili zetu sio ndogo, mie naomba tusahau yaliyopita kwa kujua pengine tulikosea na sasa tuangalie ni vitu gani tunaweza kujifanyia au kuvifanya ili tutoke hapa tulipo. Mafanikio katika hili ndiyo lingekua jibu zuri kwa hizo hoja za upungufu wa akili za mtu mweusi.Kapongola Tarehe: 28/11/07 2:59 PM, anonbinafsi kuna maswala yananitatiza sana!1:kwanini nchi tuzazoongoza sisi waafrika ni maskini na hakuna maendeleo?angalia afrika ya kusini kabla ya mzee mandela na baada ya mandela!huduma nzuri na bora za afya,elimu,usafiri,hoteli ni zile zinazotolewa na watu weupe je sisi wa afrika tatizo letu ni nini?nchi zetu zina kila kitu lakini poor!umasikini wetu tunawalalamikia wazungu!rasilimali tukishindwa kuziexploit tunawalalamikia wazungu!tunashindwa kutumia misaada,mikopo tunawalalamikia wazungu!uchu wa madaraka,udikteta,tamaa,ubinafsi,kutojali maslahi ya walio wengi(taifa)mfano kashfa kama za richmond,rada,buzwagi wakati nchi hii ni maskini wa kutupwa je hili nalo tunawalalamikia wazungu?sisi watu weusi lazima tuna matatizo ya kuwa na IQ ndogo na akili fupi/finyu.labda hii ndiyo wameitumia kupima IQ za sisi watu weusi na kuhitimisha kuwa ni ndogo. Tarehe: 2/12/07 12:05 AM, AnonymousMlalahoi mbona haujatoa hizo link hadi sasa? Fanya hivyo tafadhali,Hata hivyo hizi link zifuatazo zinaweza kutoa mwanga kidogo kuhusu mada inayozungumziwahttp://www.lagriffedulion.f2s.comhttp://www.africancrisis.org/ZZZ/ZZZ_News_008429.asphttp://en.wikipedia.org/wiki/Race_and_intelligence