Taarifa kutoka taasisi moja ya utafiti nchini Marekani imekadiria kuwa kuna Waislamu bilioni 1.57 ulimwenguni ambapo asili mia 60 ya idadi hiyo iko bara Asia.
Utafiti huo wa taasisi hiyo Pew Forum on Religion and Public Life, umechukuwa miaka mitatu kukamilishwa ikiwa pia umejumuisha hesabu za watu kutoka nchini 232.
Imeonekana kuwa asili mia 20 ya Waislamu wanaishi Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika.
Utafiti huo pia umeonesha kuwa kuna Waislamu wengi zaidi nchini Ujeremani kuliko walioko nchini Lebanon na wengi zaidi Urusi ikilinganishwa na waislamu walio katika nchini mbili za Jordan na Libya kwa pamoja.
Idadi hii kwa mujibu ya afisa mkuu wa Taasisi hiyo imewashangaza sana kwa kuwa ni kubwa zaidi ya ilivyotarajiwa .