Thursday, October 15, 2009

HUYU NAE ATASTAAFU KABLA YA KUMALIZA UJENZI?????




Huwezi kusimama kando ya hiyo katuni, na kumeza tu ujumbe wake! Nafikiri katuni ni lazima i-“reflect” ujumbe hasa (the medium is the message)! Ni lazima kukosoa kikatuni!Kuna nyumba inajengwa na huku kuta zinabomoka. Kuna mjenzi anaweka paa (JK) kwenye nyumba yenye kuta zilizobomoka. Kuna watu wawili wanaiba matofali: Mmoja ni "Ufisadi". Wa pili ni "Umasikini". Ujenzi sasa miaka 46.Na huyo mtu aliyesimama kando ya nyumba hiyo akisema, “Na huyu pia atasitaafu bila kumaliza ujenzi!”Ndio. Kuna ujumbe wa maana, kama ulivyoshauri, “Lengo la katuni hii, nafikiri ni kutupa wazo la kuhusiana na uhuru wetu, kwamba tumejenga nini na tumehitimisha nini????.Je, katuni hiyo ni “relevant and reliable instrument” ya “kutupa wazo la … tumejenga nini na tumehitimisha nini” tangu uhuru wetu miaka 48 iliyopita? Hapana. Katuni ni "incongruous"!Kuna mengi tuliyo-“jenga” na ku-“hitimisha” kutokana na uhuru wetu wa miaka 48 kuliko hayo machache ambayo huyo “katunisti” amechora na kuyaandika.Bila shaka JK atasitaafu “bila kumaliza ujenzi”! Ndio maana yangu ya kusema kuwa “ujenzi wa taifa ni “a long-term process.”Nitaongozea kwa kusema kuwa“procees” hiyo ni “exponential” na ina-“transcend the office-duration of any incumbent President” wetu na pia uhai wake.Hatuna budi kupambana na ufisadi na umasikini wetu, kama hiyo katuni inavyojaribu kuzungumza, ingawa matatizo ya kutomalizika kwa ujenzi huo ni mengi!Lakini kupambana na hayo mawili yaliyotajwa si “panacea” ya kujikwamua kutokana na hayo yaliyotufunga jelani.Kila mara huwa najiuliuza, “Je, kweli tutauzika umasikini? Ningependa kusikia kutoka kwa wanakijiji!Kuna nchi ambazo zimejengeka kwa karne, na karne, na karne zilizopita! Nyingine toka enzi za ma-Visigoth na ma-Viking; toka enzi za William the Conqueror, toka enzi za George Washington, toka enzi za Bonaparte, na kadhalika. Lakini mpaka leo hii ufisadi na umasikini bado vimejikita katika baadhi ya nchi hizo. Sembuse miaka karibu 50!Najua leo hii Tanzania ina bahati kubwa ya kuweza kuruka karne nyingi za majaribio. Viongozi wetu budi waamuke ili miguu yetu iende pamoja!Mguu wetu mmoja umo katika mazingira ya nchi zilizoendelea – walalaheri wenye maisha “tambarare”; mguu mwingine umejikita katika matope ya mazingira ya maisha ya enzi za wawindaji na wachuma mwituni (foragers) – walalahoi zaidi!

Blog Archive