Wednesday, February 16, 2011

kitabu cha mashairi ya nkya85..kipo njiani kutoka ...usikose copy yako....







ULIMI UMEPONZA KOKWA LANGU

Naanza kwa masikitiko,huzuni na kwa majonzi

Wasemavyo waendako,limezuka kwa mapozi

Ladunda mpaka kwako,kwa futa la vipodozi

Maneno kweli matamu,ulimi na kokwa langu





Lasababishwa na dudu,du lisiloonekana

Hatari kwa wazee du!,watoto na kwa vijana

Mwalimu ashanga dudu,lapita kidato tena

Mwalimu ashtuka du!sugu gojwa limechapa



Jinyoshe mpaka kesho,ni yule yule mrembo

Mwili watoka kijasho,jeba kwa shipa hajambo

Asha na zaina kesho,hulindiwa kwa viumbo

Jifunze kusema nehi,taepuka gonjwa hili



Homa za mara kwa mara,tapika hadi utumbo

Ataka nasaa bora,kwa kufuata mkumbo

Zungu aweka mipira,yamshinda juu ya tumbo

Jifunze kusema ode,taepuka gonjwa hili



DAGAA NAE SAMAKI MAJI HAYAMPONYOKI

Dagaa nae samaki ,maji hayamponyoki

Aendapo hashikiki ,kucheza kwenye visiki

Hata upige fataki ,kwenye maji hashikiki

Usimuinde samaki,tapoteza muda wako

Samaki chakula chake ,ni majani na utope

Haachi chakula chake ,kamwe hata kama tope

Akikosa ndugu zake ,humpa hata mapepe

Samaki ndio bahari,huwezi kutenganisha

Wengineo binadamu,huingilia ya ndugu

Baadae hujilaumu,kwa kuonekana gugu

Mshikamano wa damu,wezi tia lako gugu

Chukua jembe ulime,acha gomvi la ndugu

NACHAPA KWA ULIMI



Naombeni masikio ,nataka toa moyoni

Nimekolea kileo,kilicho jaa moyoni

Nichukuwapo kioo, namuona kiyonini

Binti huyu bambataa,na wala si chakubimbi



Ninapokutana nae,mdomo hujaa kete

Namuachia pekee,seme mpaka atete

Chakula nimtengee,yake maji nikalete

Nampenda misi wangu,kwa uturi anipao



Mapenzi kwangu uhai,kila mara hukinai

Kama ninywae divai,baridi katika kuzi

Laiti si kitu hiki.,pangekuwa pana dhiki

Dunia singekalika, kwa uzito wa majonzi



Angalia macho yangu, kamwe hutokuja juta

Machozi kwangu pingu,hayawezi kukupata

Njoo kiumbe wa Mungu,tukoge tulivyopata

Wangu mzizi nibebe, tufike matawi ya ju



ELIMU YA BINADAMU NI
GARI MOSHI



Yatabarizi makala ,kwa nguvu zake manani

Kalamu naanza kala ,aliyo juza manani

Mengi wakati kulala,mengine ulimwenguni

Ajuza nyingi elimu,mazingira mbalimbali





Mzazi ndie wa kwanza,elimu aliyotoa

Nyumbani ndipo kwanza,elimu inaponzia

Rejea nyumbani kwanza,mizengwe yapotokea

Elimu yenu wazazi,dunia wetu msingi





Mzazi sipokujuza ,mwalimu atakujuza

Dunia vingi hujuza ,mwalimu nae akuza

Wosia wake sikiza ,ndoto zako zitakoza

Heshima yako mwalimu,manani akujalie





Mwalimu sipokujuza,vya habari vitajuza

Disko washwa bonyeza,wimbo utasikiliza

Runinga raha bonyeza,utamu vingi kujuza

Redio gazeti mwee,udaku tajipatia





Disko napochanganya ,warika watakujuza

Jifunze mengi ya kunya,warika kweli wakuza

Weza tembea na nyanya,warika napo kujuza

Washikaji kweli noma,mtaa nimeujua

Blog Archive