Thursday, January 13, 2011
Usilie kwa ajili ya mapenzi mpira ni dakika 90....
NI wiki nyingine tunakutana kupitia safu hii nikiamini kwamba kwa rehema zake Mwenyezi Mungu umzima na unaendelea vyema na shughuli zako za kila siku kama kawaida. Mimi nashukuru naendelea vizuri na majukumu yangu likiwemo hili la kukuandikia mada ambazo kwa namna moja ama nyingine zinagusa maisha yako ya kila siku hasa linapokuja suala la mapenzi. Wiki hii nataka kuzungumza na wale ambao mapenzi yamekuwa yakiwafanya wakose raha kabisa katika maisha yao na kufikia hatua ya kukufuru kwa kutamka maneno yasiyofaa. “Jamani nimemkosea nini Mungu mimi? Yaani nimekuwa mtu wa kulizwa kila siku kwa sababu ya mapenzi. Mbona rafiki zangu wametawaliwa na furaha katika maisha yao, mimi nina kasoro gani?” Haya ni maneno ambayo unaweza kuyasikia kutoka kwa msichana au mvulana ambaye ameona mapenzi hayamtendei haki. Lakini sasa kuna jambo nataka kulisema kwa wale ambao wako katika hali hiyo. Kwanza, tufahamu mapenzi yanaua! Hilo halina ubishi. Wapo waliojikuta wanaumwa vidonda vya tumbo na mwishowe kufariki dunia kwa sababu ya mapenzi. Wapo waliodiriki kujiua kwa sababu wamekataliwa au wametendwa na watu waliotokea kuwapenda kupitiliza. Kwa kifupi, mapenzi ni kitu ambacho kila mmoja anatakiwa kuwa makini nacho kwa kuhakikisha hakiyaathiri maisha yao ya kila siku. Tunatambua kwamba kila mmoja ana moyo wa kupenda lakini sasa tunatakiwa kuangalia mahali pa kupenda. Siyo kila wakati tuuachie moyo ufanye maamuzi, wakati mwingine moyo wako unaweza kukuingiza kwenye matatizo kwa kujikuta unapenda pasipo na penzi, mwishowe ukawa ni mtu wa kuumizwa kila siku. Labda tuangalie mambo yanayowafanya baadhi ya watu kuwa ni wa kutoa machozi kila siku. Kwanza kulia kutakuwa hakuepukiki kwa mtu yoyote endapo atakubali kuangukia kwa mtu asiye na mapenzi naye. Hivi furaha itatoka wapi kama kweli mtu uliyemkabidhi moyo wako atakuwa hajakupa nafasi katika moyo wake? Ni wazi utalia kwani kusalitiwa itakuwa ni jambo lisiloepukika, kupuuzwa, kutothaminiwa pamoja na kutooneshwa mapenzi ya dhati. Pia unaweza kutokea kumpenda mtu flani ambaye naye anakupenda lakini hajatulia. Watu wa aina hii wapo huko mtaani. Yaani anakupenda wewe lakini bado haridhiki na kile anachokipata kutoka kwako. Matokeo yake naye anakuwa mwepesi wa kukusaliti na hata pale unapokuja kugundua, hujuta sana na kuomba msamaha kwa kulia kuonesha kuwa, alichokifanya hakitokani na kutokukupenda, bali ni tamaa zake. Ndiyo maana mara kwa mara nimekuwa nikisema, mapenzi ni sawa na kucheza kamari. Nikimaanisha kwamba, unapotokea kumpenda mtu utarajie mawili, aidha na yeye kuwa anakupenda au hakupendi. Itakuwa ni hatari sana endapo utakayetokea kumpenda atakuwa hana hata chembe ya penzi kwako lakini akakukubalia kwa kukutamani tu. Hapo tarajia maumivu. Hata hivyo, hayo yote ni maisha, mwisho wa siku unatakiwa kujua kwamba, binadamu mwenzako hana nafasi ya kukukosesha furaha. Kila jambo anapanga Mwenyezi Mungu. Hivyo basi, kama leo hii huyo uliyenaye anakusababisha uchanganyikiwe kiasi cha kutoona furaha ya maisha, unatakiwa kuamini kwamba hayo ni mapito na siku za furaha zinakuja kwako. Mungu siku zote hawezi kumtupa mja wake, hata kama leo hii mapenzi yanakutesa, usione kwamba Mungu kakutupa, usidhani Mungu hayaoni machozi yako. Yawezekana anakupa mtihani wa kukupima kisha aone utafanya nini au utasema nini. Wewe jiulize kwamba kwani ni lipi ambalo umemkosea mpaka awape furaha wengine wewe akufanye mtu wa kulia kila siku? Kubaliana na hali hiyo kwa sasa lakini amini siku si nyingi machozi unayotoa yatabaki historia hapo baadaye. Sisemi hivyo kwa kukutia moyo tu bali hata wewe mwenyewe utakuwa umeshuhudia watu ambao huko nyuma walikuwa kama wewe lakini leo hii ni watu na wapenzi wao, ni watu na waume/wake zao, tena katika maisha mazuri. Kwa sasa endelea kucheza kamari. Kama moyo wako umempenda mtu fulani, endelea kumpenda na kama atakuwa anakutenda, vumilia katika yale yanayovumilika. Ukiona amezidi na moyo wako unasita kuendelea kuwa naye, hata bila kuomba ushauri kwangu au kwa mtu mwingine, muweke pembeni kisha ishi maisha yako. Jamani kwa leo naomba niishie hapo nikiamini kwamba wale wanaoteswa na mapenzi, nimepandikiza mbegu mpya katika mioyo yao. Tujiepushe tu na kusema, ‘mimi sitakuja kupenda tena’ eti kwa sababu mtu uliyekuwa naye kakutenda. Huwezi kuishi peke yako milele, mwenza ni kitu muhimu katika maisha na kumbuka uliye naye sasa siye ambaye utampata kesho, watu wanatofautiana
Blog Archive
-
▼
2011
(1531)
-
▼
January
(66)
- Rango: behind the scenes
- Cheka...urefuke..
- [New]working on watchersnplayers.tk/
- Sijaona cha kukupa duniani...labda Mungu kakuandal...
- Huyu binti ndie aliyeongoza matokeo ya kidato cha ...
- Bahari ambayo mtu hawezi kuzama
- Noti mpya tz zamwaga rangi ..angalia usivae na sut...
- lets be quite...
- Ona kokwa upande wa ndani...
- hebu ona huyu ****alivyochojoa...
- Huge New Dive Attraction for Cayman Islands
- Is katrina kaif the princess of popcorn?
- ''Baba wa taifa akirudi tena kwenye hii nchi tz..a...
- Ajifungua mkono mzima ....madaktari hoi...
- Disney's California Adventure® Overview
- We Are The Caribbean - Sandals Resorts Chairman & CEO
- Transatlantic Crossings
- 50 States & 50 Vacations (Alabama to Massachusetts)
- New Cruise Ports
- High-End Car Rentals
- Snoop dogg -wet
- Kanye West Buys $180k Watch of Himself!
- Usilie kwa ajili ya mapenzi mpira ni dakika 90....
- Huamini nini !!!...yule demu huyu hapa....!!!!?
- ukimaliza kuangalia na kusoma omba dua .....!!!
- Get Your Passport Some Action
- Contiki...A trip of a lifetime!
- Southern States Vacation
- Aussie Word of the Day!
- Economical Excursions
- Travel and Leisure Top 5 Hotels for 2011
- Fiji: welcome to paradise.
- Harry Potter: Orlando, FL
- Nature's Light
- All-Inclusive Resorts in Negril, Jamaica
- 3d Work by Jules
- FACEBOOK WILL END ON MARCH 15th!
- 10 Reasons why you should use a Travel Agent!
- British Honduras
- Titanic Museums and Exhibits
- Luxury Cruises
- comin home .....welcom Diddy
- The Bahama's (Caicos to Nassau)
- Amitha Bachchan anakula bata kwa kwenda mbele..
- Weddings and Honeymoons Blog
- Learn Italian (Language and Culture)
- Restaurants With A Fireplace.
- Every one has his dream........ze comedy corner
- Vimeo.........produ..........
- kina nini...kiuno???,....kifafanue....
- Jamani mchumba wa Dr..Slaa.....!!!!
- ''Napendwa na wanawake mpaka nawaomba wapunguze''
- breaking nyuuuuuuuu.Z.....A.TOWN KUMENUKA...JIONI ...
- kikwete mikononi mwa Bi kidude....Moshi washangaa
- The best of London, Paris & Rome
- Man-Made
- Strange Monuments
- Je.unajua ni kwanini wakina*****wanatembea na pich...
- Naipenda mimba kuliko mtoto mwenyewe....
- ziplining in Catalina Island California
- National Chocolate-Covered-Cherry Day
- Travel to Vietnam
- Cancun Tours
- Film Locations
- As seen on TV.
- Msiba wa mtanzania Hyderabad india
-
▼
January
(66)