Monday, August 30, 2010

TANZANIA YACHUKUA KIKOMBE CHA MASHINDANO YA RAMADHANI MJINI HYDERABAD KILICHOANDALIWA NA JUMUIYA YA WANAFUNZI F.S.A INDIA 2010

Mashindano haya yanaandaliwa na jumuiya ya wanafunzi wa kigeni mjini Hyderabad kila mwaka ifakapo mwezi wa kiislam ramadhani.Mwaka huu jumuiya ya wanafunzi wa kitanzania (T.S.A.H) mjini hyderabad india waliingiza timu yao,katika kinyang'anyiro cha kombe hili la mwezi huu wa ramadhani.Ambapo timu ya Tanzania iliibuka kuwa mshindi baada ya kuizaba timu ya ELTREA 1-0.Hivyo kuibuka mshindi ktk kinyang'ang'anyiro cha kombe hili
Hawa ni wachezaji wa timu ya tanzania wakishangilia baada ya kupewa kikombe hichi,ktk mechi ya kwanza tanzania ilicheza na timu ya cameron ikashinda 4-3 ambayo yalikuwa ni magoli ya penati,na ktk mechi ya pili ilitoka Tanz 2-1 Sudan ,mechi ya tatu Tanz 3-1 AFGHANSTAN hivyo baada ya kuizaba timu hizo ndipo fainali walipokuja kuizaba tena ELTREA 1-0
KWA KWELI ILIKUWA PATA SHIKA NGUO KUCHANIKA MASHABIKI PAMOJA NA WACHEZAJI WALISHANGILIA SANA ..KWANI TOKA MASHINDANO HAYA YA RAMADHANI YAANZISHWE TZ HAIJAWAHI KUCHUKUWA KIKOMBE HICHI HII NI MARA YAKE YA KWANZA JAMANI TANZANIA TUKO JUUUUUUUUUUUUU
WATZ WAKISHANGILIA PIA KWA KUPEPERUSHA BENDERA YAO YA TAIFA KUONESHA UALENDO WAO WALIJIWEKEZA KTK NCHI YAO
KULIA KWAKO NI M/KITI WA JUMUIYA YA WANAFUNZI HYDERABAD INDIA ALIPATA PIC MOJA YA UKUMBUSHO NA TIMU YA TANZANIA
HUYU NI MAKAMU M/KITI WA JUMUIYA YA WANAFUNZI HYDERABAD LKN PIA NI MCHEZANI WA TIMU YA TZ HAPA AKIPONGEZWA NA MGENI RASMI BAADA YA KUIPATIA TIMU YKE USHINDI
Mchezaji wa kitanzania Bw Foba akipongozwa na mgeni kwa kazi nzuri walioifanya ..baada ya kuipatia yimu yao ushindi
Hizi ni baadhi ya jezi ambazo timu yetu iliwezwa kuzawadiwa baada ya kupata ushindi huu
Hapa watanzania wakishereheke ushindi wao
baadhi ya watanzania waliojitokeza kuangalia mpambano
Mwenye fulana nyeusi ni M/kiti wa jumuiya akiwa pamoja na wenyeviti wa nchi mbalimbali hapa mjini Hyderabad
kinadada wa kitanzania pia hawakuwa nyuma kushangilia ushindi wao
hapa wachezaji wa kitanzania wakipokea medali zao a ushindi

watz kazi nzuri sana ...
Mkiti wa kamati ya starehe Dani msemo akibusu kikombe kuonesha ishara ya ushindi tulioupata ..kijana..na hizi pics hapa ni mchakato wa huyu mheshimiwa kazi nzuri kijana mchakato mzuri
Mkiti wa jumuiya Bw Abdillah akiwa na wanajumiya kushangilia ushindi uliopatikana

HUYU NDIE MCHEAJI ALIYETUZABIA BAO LA USHINDI Bw Said Mihala hapa akipewa medani ya ushindi..kazi nzuri kijana unastahili zawadi
KWA KWELI WATZ WALIFURAHI SANA
KINADADA WA KITANZANIA WAKISHANGILIA USHINDI
HAPA ILIKUWA KABLA YA KUPEWA KIKOMBE CHAO ...WALIKUWA WAKISUBIRI KWA HAMU SANA
M/kiti wa jumuiya Bw Abdillah nkya akiwa na kipa wa tanzania Bw RAHIMU pamoja na Bw SHAKIR Wakiashiria tuko pamoja
Huyu ndie meneja wa timu ya tz hapa mjini hyderabad Bw enock akijimwagia maji baada ya kumaliza mechi
HAWA NI VIJANA WANAOKAA KARIBU NA UWANJA WA MASAB TANK ULIOCHEZEWA MECHI HII HAPA HYDERABAD WAAKAA KITONGOJI CHA TOLICHOKI WALISEREBUKA KUPITA KIASI
KWA KWELI WATZ WALIJITOKEZA KWA WINGI KUJA KUANGALIA MPAMBANO HUU HAPA MJINI HYDRABDA UWANJA WA MASAB TANK
kijana Dani msemo akionesha uzalendo na nchi yake yatanzania baada kuipeperusha bendera ya tz uwanja mzima
siku hii watz walipiga sana mavuvuzela
kwa kweli watz waliserebuka vya kutosha ktk kusherehekea ushindi huu...yaani kulichezwa bolingo la kufa mtu............

Blog Archive