Wednesday, August 4, 2010
HOTUBA YA JANUARY MAKAMBA BAADA YA KUTANGAZWA KWA MATOKEO YA KURA ZA MAONI YA UBUNGE JIMBO LA BUMBULI KWA TIKETI YA CCM ILIYOTOLEWA KATIKA UKUMBI WA O
CCM Oyee! (Oyeee!)
CCM Oyee! (Oyeee!)
Bumbuli mpoo? (Tupoo!)
Nashukuru sana.
Sasa, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa rehema zake. Tupo tumefika hapa leo tulipo kwasababu ameamua iwe hivyo. Ametujalia uhai, uzima na afya kati yetu. Kwahiyo ni muhimu kumshukuru.
Pili, napenda kuwashukuru wazazi wangu kwa malezi mazuri, kwa mchango wao mkubwa kwenye maisha yangu mpaka nimefikia hapa nilipofikia leo. Pia familia yangu – mke wangu na wanangu wawili – bahati mbaya hawapo [hapa] – wamesafiri. Lakini nawashukuru kwa kunitunza, kwa kukubali kukabiliana na hizi presha za siasa, na kuniunga mkono na kuwa na mimi wakati wote.
Lakini vile vile namshukuru bosi wangu, Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Namshukuru kwa kunikubalia nimtoroke kidogo kazi na kuja kufanya huu mradi, na namshukuru kwa ushauri na malezi ya kisiasa aliyokuwa akinipa wakati wote.
Lakini sana sana, nawashukuru wana-CCM wa Bumbuli kwa kuniamini - kwa kuniamini kwa kiasi kikubwa namna hii kwa kunipa kura nyingi sana. Waswahili wanasema, “Imani huzaa imani”. Imani waliyonipa kwa kura wanizonipa ni kubwa sana. Tutasherehekea leo, lakini kesho tutakumbuka kwamba kura hizo ni…maana yake ni kwamba wanategemea mengi kutoka kwangu. Na mimi naahidi kwamba sitawaangusha. Nitaibeba bendera ya Chama chetu cha Mapinduzi, na kuipeperusha na kuinadi Ilani yetu kwa uwezo wangu wote, kwa maarifa yangu yote na vipaji vyangu vyote nilivyojaliwa na Mwenyezi Mungu. Na naamini kabisa kwamba Chama chetu kitapata mshindi mkubwa sana kwenye jimbo la Bumbuli.
Lakini pia ningependa kuwashukuru wenzangu - wagombea wenzangu tulioshiriki nao, kwa kuonyesha ustaarabu mkubwa. Tumevumiliana, tumeheshimiana kwenye mchakato mzima. Ndugu yangu Kaniki mmemuona mwenyewe ni kijana mzuri, amekomaa vizuri.
Mzee Shelukindo – naomba niseme machache kuhusu Mzee Shelukindo, bahati mbaya hayupo hapa. Lakini kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi. Leo wana-CCM wameamua… jana wameamua, kwamba mwingine apeperushe bendera ya Chama chao kwenye uchaguzi mkuu. Lakini heshma ya Mzee Shelukindo katika nchi yetu bado ipo pale pale (makofi). Kwa kushindwa kura hizi za maoni, haina maana kwamba heshima yake na rekodi yake ya utumishi imepotea kabisa. Hapana. Ni maamuzi ya wanachama. Binafsi nitaendelea kumuheshimu kama Mzee, lakini [pia] kama kiongozi wa muda mrefu kwenye Serikali. Ni hazina kubwa ya uzoefu kwenye jimbo letu, na bado ni mwanachama wa CCM. Na binafsi nitaenda kumuomba rasmi…hatujakutana tangu tumalize mchakato huu, lakini nitamtembelea nyumbani kwake kumuomba kwamba tusaidiane kikazi (makofi).
Lakini naomba niwashukuru wapiganaji wangu walionisaidia kunadi jina langu. Walionisaidia kuwashawishi wana-CCM wa Bumbuli kwamba mimi nafaa. Nawashukuru kwa kazi nzuri. Ushindi huu uliopatikana ni matunda ya kazi yenu. Lakini vile vile naomba niwaambie kwamba uchaguzi umekwisha jana. Mpambano umekwisha. Sasa hivi sote tunarudi kwenye hema la Chama chetu cha Mapinduzi. Sina uadui na Mzee Shelukindo. Sina uadui na Bwana Kaniki. Sina uadui na Mzee Mshihiri (makofi). Sina uadui na mtu yoyote aliyeshiriki kwenye mchakato huu.
Kwahiyo wapiganaji wangu, nawaomba sana sana sana tuache tambo. Tuache kutambiana. Uchaguzi umekwisha jana. Kazi ya kunipigania imeisha, tunaanza kazi ya kukipigania Chama chetu. Ndio kazi iliyo mbele yetu, na naomba tuifanye kwa umoja, tukishirikiana na wale ambao hawakuniunga mkono kwenye mchakato huu. Kwa nguvu ile ile ambayo mlinipigania mimi, naomba sasa nguvu hiyo muielekeze katika kukipigania Chama chetu kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba mwaka huu.
Naomba vile vile nitoe shukrani na pongezi zangu kwa uongozi wa Chama Wilaya, Katibu wa Wilaya na timu yake. Wilaya yetu ina majimbo matatu na kata 44. Zoezi hili ni zoezi kubwa, hasa kusimamia chaguzi za madiwani katika kata zote hizi. Ni kazi inayohitaji uwezo mkubwa, inahitaji rasilimani za uendeshaji na uwezo mkubwa wa kiutawala. Natambua kwamba zimejitokeza kasoro za hapa na pale, lakini naamini kwamba kasoro hizo zinatokana na upya wa mfumo wetu huu mzuri wa kurudisha demokrasia kwa wanachama kuchagua ni nani wawasimamishe kupeperusha bendera ya Chama kwenye uchaguzi wa wabunge na madiwani. Naamini kwamba matatizo yaliyojitokeza yatashughulikwa, na wakati ujao tutakuwa na utaratibu mzuri zaidi. Lakini vile vile naamini zaidi kwamba kasoro zilizojitokeza hazikumnyima mtu haki, na kwamba matokeo haya ya Bumbuli ni kielelezo halisi cha matakwa ya wanachama wa CCM wa Jimbo la Bumbuli.
Na mwisho, napenda kuwashukuru wote waliojitokeza hapa kunisikiliza, na nawatakia jioni njema. Nashukuru sana. (makofi)
January Makamba,
Agosti 2, 2010.
Blog Archive
-
▼
2010
(485)
-
▼
August
(29)
- Hurricane Earl on track to clip U.S. East Coast
- [MODEL + TEXTURE] Goan Church
- Jules Animation work: [Texture] Church 3D model te...
- Alaska Cruise Tour (The Weaver Family)
- [animation]Clay Animation Test
- TANZANIA YACHUKUA KIKOMBE CHA MASHINDANO YA RAMADH...
- Places to See and Things to Do (Chile)
- Where Do You Want To Go?
- Contiki Vacations are for you!
- Health and Wellness Fair
- Where should I Stay in Hawai'i?
- Then and Now Travel
- Alaska 7-Day Inside Passage Cruise
- www.facebook.com is where to find Unique Travel Co...
- World Cruises (Princess) Starting Soon
- Weekend Getaway to Monterey
- Mexico's Beaches Video
- Take A Vacation in San Diego
- Carnival Splendor, Ship Inspection, August 8th 2010
- Israel or in Hebrew "Medinat Yisrael"
- Dedicated to the Church of St Luke Holyland Group ...
- matokeo ya kura za maoni kinondoni, kawe, ubungo n...
- TAHADHARI NONDOOOZ ZA CHUMA KIMOJA.
- [pixilation] The lazy Kiddo ... v/s kaxtiman man
- KWA MTINDO HUU WANAFAIDIKA KWELI HAWA WAKULIMA ?
- HOTUBA YA JANUARY MAKAMBA BAADA YA KUTANGAZWA KWA ...
- Want to Cruise the Nile?Start with a visit to Abu ...
- the most popular woman on the web
- Quotes about Travel"The World is a book, and thos...
-
▼
August
(29)