Saturday, December 11, 2010
Mapenzi ni tendo la furaha. Wakati wa utekelezaji huwa ni sherehe tupu kwenye sayari ya vionjo vya kimahaba
Mapenzi ni tendo la furaha. Wakati wa utekelezaji huwa ni sherehe tupu endapo wahusika watakuwa wamekubaliana kwa moyo mmoja. Yaani hisia zao ndizo zilizowashawishi kuingia kwenye ‘bwawa spesho’. Kinyume chake ni mateso na ndiyo chimbuko la tuhuma za wanandoa kubakana. Utafiti unaeleza kuwa wanaume wengi huwa hawakubali neno ‘nimechoka’ ambalo ni kawaida kutamkwa na wanawake. Ni lugha ambayo hutumiwa ili kukwepa ushawishi wa wenzi wao ambao huwataka kuingia nao kwenye sayari ya vionjo vya kimahaba. Hata hivyo, lipo jibu la kitafiti kwamba asilimia kubwa ya wanawake walio kwenye ndoa ambao walijaribu kueleza hisia zao kwa ‘mamista’ wao kuwa hawapo tayari kwa tendo, walibakwa. Wakati mwingine hili hubebwa kwa tafsiri kuwa ni jambo la kawaida. Inawezekana hili likawa halipati kujadiliwa sana kwa sababu mpaka leo kuna wanawake bado wanaamini kubakwa na waume zao ni sawa. Kinachowapa unyonge huo ni imani kwamba mwanaume ana haki zote za kimsingi za kuutawala mwili wake. Ziangalieni nyumba nje ya kuta, ndani kuna mengi! “Mwanamke akiolewa haruhusiwi kulala akiwa amevaa kabati!” Ni msemo ambao unavuma mno. Kinachotajwa hapo ni kuwa anayekubali kuolewa, moja ya masharti ni kukubali ombi la mwenzi wake wakati wowote. Ni kweli? Usiku amelala, ghafla anashtuka uzito umeongezeka kifuani, kuangalia, kumbe ni mume anatimiza haja zake! Hiyo ni sahihi? La hasha! Mapenzi hayapo hivyo! Nimesema kuwa tendo la mapenzi linahitaji uhuru wa hisia. Kulazimisha ni kumuumiza. Kukwea juu ya mwenzako bila taarifa ni unyanyasaji. Kila mtu ana wajibu wa kuheshimu mwili wa mwenzake na azitangatie ‘u-tayari’. Ni vizuri kujitambua. Mfumo wa kubakana haukubaliki! Ila ni vema pia watu wakaelewa kuwa ni kosa kubwa kubania unyumba, kwani wengi wao wamejikuta wakisalitiwa kwa sababu hiyo. Yapo mambo ambayo natakiwa nikuchambulie ili kufahamu thamani ya tendo! UTAPOTEZA MVUTO WAKO Tendo ni chachandu! Kwa wanandoa au wapenzi ambao wanaliheshimu hili na kulitekeleza kwa kiwango bora, huwafanya wenzi wao wawe na hisia za karibu kila wanapowafikiria. Hii ina maana ya kuongeza mvuto! Mtu ambaye anakuwa mvivu kutekeleza, mwisho wa siku hupoteza mvuto wake. Kwa asili kila binadamu huwa hapendi usumbufu. Alihitaji penzi la amani, ndiyo maana akawa na wewe, lakini kwa kitendo chako cha kutotaka ‘kachumbari ilike’, maana yake unampa mateso aliyoyakimbia. Anakuomba leo, unamjibu umechoka, kesho tena unaweka ngumu! Hasara kwako hapo ni kupoteza mvuto wa kimapenzi, kwa maana atakapohisi kuhitaji tendo, kila akikufikiria wewe ataona ni mtata na hueleweki, kwamba akikuomba utamtolea nje. Kwa mwanamke ni hatari zaidi, kwani kwa wanaume wasio na uvumilivu, mwisho wa siku huishia kubaka. Hata hivyo, mara nyingi hiyo haiishii hapo, tatizo hukua zaidi na zaidi kulingana na jinsi mgogoro wa kuwekeana ‘kauzibe’ unavyoshamiri ndani ya nyumba. Ukiweza kumudu kumfurahisha mwenzi wako, anachokihitaji umpe kwa wakati. Maana yake atazidi kukuona lulu. Kila akiwa na wewe atajiona yupo huru kuomba huduma wakati wowote. Na pale utakaposema umechoka, itakuwa rahisi kukuelewa na kukuvumilia, kwani siyo kawaida yako. KUSALITIWA NI NJE NJE Unambania kila siku, aendelee kukusubiri kwa kitu gani hasa? Kama ni mwanaume, maua yapo mengi ‘kitaani’, kwahiyo ataangalia kwingine kwa lengo la kutuliza mizuka yake. Ni vema ukitambua kwamba huyo siyo amoeba! Ni mtu hai anayehitaji huduma. Kisaikolojia, ni mwanaume mmoja kwa mia, anayeweza kuvumilia kukaa muda mrefu bila kufanya mapenzi. Asili ya maumbile yao, hasa walio na afya timamu, hisia zao zipo karibu, kwa maana hiyo anaweza kuhitaji hata kila siku. Kama ni mwanamke, ni busara kulitambua hili. Mwanamke anaweza kukaa muda mrefu bila kutamani tendo, lakini hatari kubwa ni kwamba uwezo wake wa kuvumilia ni mdogo mno pale anapokuwa jirani na mwanaume. Akiwa peke yake ni sawa, ila akiwekwa jirani na watu wa jinsia ya pili, mambo huenda kinyume chake. Unafika nyumbani unalala mzungu wa nne, lakini kuna wakati ukigeuka na kumgusa, unamfanya ahisi kutaka huduma. Wewe unambania, hapo utamsababishia akiamka, afikirie mahali ambapo anaweza kupata tiba! Kwa muuza bucha, genge au hata houseboy! Akiitwa barabarani atakuwa mwepesi kusikiliza kwa sababu mwili wake ni mzito na unahitaji kupunguzwa. Akiulizwa kama ana mume, atajibu hana na akisema anaye ataeleza kwamba hana noma! Akiombwa namba atatoa, mwisho wa siku, haki yako atapewa mwingine. Usifikirie maumivu ya kusalitiwa, tafakari kuhusu jinsi unavyodhalilishwa. Kama binadamu na uhusiano wa kimapenzi, heshimu ya kweli ni pale ambapo mwenzi wako anakutunzia ‘tamu’ yako kwenye mazingira yoyote yale. Akiitoa, ni sawa na kuvuliwa nguo! Pale unapopumzika na wengine hutulia hapo hapo! Hii inamaana kuwa hutakiwi kujiuguza uvivu katika suala la mapenzi. Toa huduma inayotakiwa, ikibidi ongeza vionjo kadiri unavyoweza. Kosa kubwa kwa wengi ni kwamba hawachukulii tendo kama ni jukumu la kutekeleza. Yaani ni wajibu! Wanaona ni kitu rahisi ndiyo maana kila siku wanalia.
Blog Archive
-
▼
2010
(485)
-
▼
December
(42)
- The New Year
- kumbe ganda la katiba ya tz liko hivi...!!!..unaju...
- Show it ...at new year 2011!!!!!!
- Affordable Japan Vacations
- HapPy B.dAy ....Bakari Changale
- Catalina Island
- Italy and Vatican City
- rango behind the scenes
- Baada ya yote vijisenti abusu mahakama kwa laki 7
- African Safari Trips
- Tron: Legacy
- Rango: more about the movie rango
- May this season bring u success ,gud tym & happin...
- Soma chachandu ,vikuku na vichele vya Xmass na New...
- Rango another trailer
- Christmas Traditions (Germany)
- Unajua kwenye ma***nzi kuna asali, limao na shubiri?
- Rio a 3D animated movie
- Christmas in the Village
- way to ur home.....
- Places of Spiritual Importance
- WOLPER apigwa bao mchangani
- Rango 3d animated movie more stuff/preview
- Rango 3d animated movie coming soon
- Pirates of the Caribbean: On Stranger Tides
- REMMY ONGALA AFARIKI DUNIA
- Legend of the Guardians: making and tralier
- slowly here we goooooooo Dr Dre
- Mapenzi ni tendo la furaha. Wakati wa utekelezaji ...
- [3D] Ferrari Car Wheel- 3d, maya with texture
- NEW SONG BONTA.....
- Adriana Lima Models $2 Million Dollar Bra
- Namitha Kapoor is happy being single
- Great Mexico Vacations
- Extravagant Castles Around The World
- Siku tuliyopewa uhuru wetu Tanganyika 09.12.1961 ...
- Royal Caribbean Introduces the DreamWorks Experience
- Allure of the Seas: Announcing Chicago the Musical
- Celebrity Owned Resorts
- SIFA NYINGINE ZA KIJINGA.COM
- Places you should see: before they're gone.
- Tropical Destinations, no passport required.
-
▼
December
(42)