Ndugu Watanzania pamoja na Wanajumuiya ya wanafunzi
Kama mnavyojua, hali ya kisiasa katika Jimbo la Andhra Pradesh si shwari kutokana na vurugu za kisiasa za kuishinikiza Serikali ya
Kufuatia hali hiyo, Mitihani ya Semister imekuwa ikiahirishwa mara kwa mara tangu Mwezi November, 2009. Takribani miezi miwili na nusu sasa. Aidha kumekuwa na migomo ya wanafunzi (wahindi) kuingia madarasani hadi hapo Jimbo
Ni wazi ifahamike kuwa vurugu hizi ni za kisiasa na hazihusishi mwanafunzi yeyote wa kigeni (Foreign students) isipokuwa wanafundi wakihindi wanaoshabikia siasa. Hata hivyo athari za kutofanyika mitihani kwa wakati napengine kufutwa kwa mwaka wa masomo zinatuathiri wote kwa pamoja
Ndugu wanajumuiya, kuahirishwa kwa mitihani ni upotevu wa muda na ikitokea kufutwa kwa mwaka wa masomo ni usumbufu kwetu na upotevu wa gharama.
Kutokana na hali hiyo, leo tarehe 20.01.2010 Uongozi wa Jumuiya umefanya kikao cha dharura kujadili suala hili na kuamua kuchukua hatua zaidi ikiwemo kuandika barua maalum kwa Uongozi wa Chuo ili utoe msimamo wake juu ya hatima ya wanafunzi wakitanzania wanaokumbwa na athari za vurugu hizi. Pia kikao kimeazimia kulifikisha rasmi (kwa barua) suala hili katika Ubalozi wetu
Mwenyekiti wa Jumuiya anawaomba watanzania wote kuwa wavumilivu wakati huu ambao suala hili linafuatiliwa na kufanyiwa kazi. Waendelee kujisomea majumbani na kujianda na mitihani muda wowote itakapoamriwa. Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
ABDILLAH DAUD NKYA
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wanafunzi wa kitanzania